Saturday, February 10, 2024

KWA NINI TUNAUGUA?


·         Kuugua ni ile hali ya kutokuwa vizuri kwa kiumbe hai. Ugonjwa/maladhi ni ile hali ya mvurugo katika utendaji wa kawaida wa shughuli za mwili na roho, inayoathiri usitawi, starehe na furaha ya kiumbe hai.

 ·         Kutokana na magonjwa kiumbe hai huyu hasa binadamu anaathirika maeneo makuu haya;-

 -          Kiuchumi – biashara, kilimo, ufugaji n.k.

-          Kimwili – kushindwa kutekeleza majukumu

-          Kiroho – huongozwa kutegemea mawazo ya watu

-          Mahusiano – kuachwa, kutekelezwa, kutengwa.

 ·         Sayansi ya tiba inasema magonjwa ya bianadamu asili yake ni kama ifuatavyo;-

(i)                 Magonjwa ya kurithi

(ii)               Magonjwa ya kuambukiza

(iii)             Magonjwa yatokanayo na ajali

(iv)             Magonjwa ya dutu za nje ya mwili kama vile;- sumu asili, mionzi n.k.

(v)               Magonjwa yatokanayo na tiba au kinga maradhi.

(vi)             Magonjwa ya nafisi na roho

 

·         Nami katika kuyaeleza nimeyagawanya katika makundi yafuatayo;-

a.       Magonjwa ya kipepo

b.      Magonjwa ya kuambukiza

c.       Magonjwa ya siku za mwisho

d.      Magonjwa ya mitindo ya maisha

MAGONJWA YA MITINDO YA MAISHA

·         Binadamu ameumbwa kwa namna ya ajabu sana kama ambavyo vitabu vya Mungu na sayansi imebainisha.

·         Hivyo binadamu akiishi kinyume na alivyoumbwa kupelekea kuathirika na kuugua.

·         Ikitokea ukala na kunywa tofauti na ulivyoumbwa basi ni rahisi kuugua na ukikosa kula na kunywa kama DNA zako zilivyopangiliwa na viumbe wengine basi tegemea kuugua.

·         Kwa hiyo magonjwa ya mtindo wa maisha hutegemea mahusiano yako katika kula kunywa kuona, kusikia na kuhusiana na viumbe wengine.

·         Mahusiano hasi na viumbe wengine hupelekea kiumbe hai huyu kuugua kama ilivyo mahusiano chanya(+) na viumbe wengine huchangia kuondoa/kuzuia maladhi kwa binadamu.

·         Mfano kuna baadhi wamepatwa na maladhi kama vile magonjwa ya moyo (HEART DISEASE) kwa sababu tu ameishi na Mke/Mme/Ndg/Rafiki ni mwenye athari HASI (-). Endapo wasingeishi pamoja au wakitengana basi ndugu huyu atakuwa na afya nzuri.

·         Sasa kupitia makundi ya damu haya kama utakavyoona itakusaidia kuepuka baadhi ya maladhi maana utajua vyakula vya kuepuka, watu wa kuepukana nao na namna ya kula na kuishi nao. Mfano;- ikitokea ndoa imefungwa mwanaume ana kundi lolote la damu lenye +RH na mwanamke ana kundi lolote la damu lenye –RH basi hawana uwezekano wa kupata mtoto na kama watafanikiwa kutungisha mimba, basi inaweza kuharibika wakati wowote, hata kama atazaliwa yuko hatarini kupoteza maisha kabla ya kufikisha umri wa miaka mitatu.

·         Ikitokea akakua bado upo uwezekano wa wazazi kutopata mtoto mwingine.

·         Ndiyo maana ikiwa mmeoana watu wenye sifa hizo hapo juu, basi ni vema kwenda kwa dakitari wa magonjwa husika kupata ushauri ili muda ukifika a[ate chanya A.NT D.

·         Pili ikitokea wamefanya mahusiano na kuingia kwenye ndoa watu wenye makundi ya damu yasiyoendana kitabia basi ni rahisi hawa watu kuishi kwa malumbano, ambapo matokeo yake yanaweza kuchangia mmoja kupata na magonjwa kama vile;-

-          Magonjwa ya moyo

-          Kujinyonga

-          Magonjwa ya mifupa

-          Magonjwa ya upungufu wa kinga mwilini.

 

-          Inapotokea watu waliofunga ndoa na kutofautiana makundi ya damu hii haisababishi kukosa watoto.

-          Ila Ikitokea wanandoa hao wametofautiana (RHESUS, FACTOR) hapa upo uwezekano wa kukosa watoto kama nitakavyofafanua hapa chini.

-          Mfano: Mtu anapokuwa na kundi la damu liitwalo (ANEGATIVE basi huitwa RHESUS factor negative.

-          Kama ikitokea mama ana kundi lolote la damu negative na baba akawa na kundi lolote la damu positive basi wawili hawa lazima watapata changamoto ya kupata watoto.

-          Kwani mimba inapotungwa wakati wa mchakato wa makuzi tumboni kinga ya mama hushambulia kijusi cha baba kama adui.

-          Ikitokea mimba hiyo ikakua basi haitaendelea vizuri itapata changamoto kadhaa zitakazopelekea mimba kuharibika au motto anapozaliwa anaishi chini ya miezi mitatu maana anaweza kufariki kabla ya kuvukisha umri wa miezi mitatu.

-          Kwani pia damu ya baba kama ni chanya na mama ni hasi basi inapoingia kwa mama husababisha mama atengeneze Antiboard dhidi ya mtoto.

 

MAKUNDI YA DAMU NA TABIA - KUNDI ‘A’

TABIA – MAZURI YAO

Hupenda ukamilifu wa mambo wa hali ya juu sana.

Ofisini na nyumbani huweka kazi, vyombo nk kwa mpangilio.

-          Hutumia vitu kwa bajeti

-          Ni waaminifu sana

-          Kwa asili ni wapole

-          Ni kundi la watu nadhiru.

-          Ni wapatanishi wazuri.

-          Ni watulivu katikati ya migogoro

-          Hutumia akili sana kufanya mambo.

-          Ni washauri wazuri.

-          Wako tayari kubeba majukumu.

TABIA – MADHAIFU YAO

-          No wasumbufu sana

-          Wana hisia kali hata kwa vitu vidogo

-          Ni watu wa gharama sana hasa wadada.

-          Hawatoi msaada wa mawazo, kama hajashirikishwa

-          Ni wakimya kupita kiasi.

KIJAMII

-          Ni wa kuaminika na kutegemewa (vipawa vizuri)

-          Anajali toka moyoni (Hawana usanii)

-          Hawapendi ugomvi, misuguano na vurugu

-          Hawapendi sherehe pia hawapendi kukaa sehemu zenye makelele hasa ya watoto.

KAZINI

-          Hutekeleza majukumu kwa usahihi na ufanisi

-          Wanajali hata vitu vidogo sana hivyo hujikuta wanapatwa na musongo sana

-          Ni ngumu sana kuwaelewa maana mambo yao hayako wazi sana maana ni wasiri.

-          Akiwa maafisa utumishi, taasisi au idara hufanya vizuri sana

-          Ni viongozi wazuri sana

-          Akizuiliwa kutimiza malengo hukaa kimya atafute njia mbadala kutimiza

 

MAHUSIANO NA MAPENZI

-          Ni wagumu kufunguka (Hawezi kuonyesha hisia haraka). Hivyo sio rahisi kuonyesha ukubali.

-          Hawako tayari kutoa historia yake ya mahusiano yaliyopita na yajayo.

-          Hakushirikishi mambo yake anataka uone tu matokeo

-          Wanapenda kujificha, hata usiku hupenda kukaa gizani. (Kwenye starehe hupenda faragha)

-          Hawapendi misuguano hivyo ni rahisi kuachika na kuacha

-          Mahusiano kati yao na group O ni ngumu kuishi kama mke na mme.

-          Sio wazuri kugawanya upendo (Hawana mahusiano ya kimapenzi na zaidi ya mtu mmoja)

-          Huumia sana pale anapojikuta ameingia kwenye mahusano na mtu wa pili wakati ana ndoa

-          Wanaume hujari mwonekano wa usafi (Huvutiwa sana na wanawake wasafi)

ZIADA YA KITABIA

-          Ni watu wabunifu sana wenye ujuzi (wanasayansi wengi hutoka kundi hili)

-          Wanalewa kilahisi sana na akilewa ni msumbufu sana.

-          Hawawezi kuingilia mazungumuzo kama hajahusishwa maana ni wakimya

-          Wana huruma sana na hupenda kusaidia

-          Wadada wa kundi hili wana aibu sana hivyo sio wachunaji kwenye mahusiano.

 

GROUP ‘A’ - KIAFYA

-          Hawa ni VEGETARIAN hivyo hujitaji mlo wa 45% uwe ni mbogamboga na matunda hasa nanasi na Zabibu, limao, nyanya, pasioni na jamii zake.

-          Hawatakiwi kula nyama nyekundu kwani ndilo kundi pekee linalizalisha asidi kidogo sana.

 

VYAKULA WASIFOHITAJIKA KUVITUMIA

-          Nyama nyekundu, hasa mweupe, sembe ngano, maziwa, vyakula vya mafuta, protini nyingi n.k.

-          Hawatakiwi kutumia kileo cha aina yoyote.

 

ZIADA KIAFYA

-          Wakitumia maembe na mapapai huwa na makamasi mengi hasa asubuhi.

-          Wanawake wa kundi hili hupata hedhi mara mbili hasa awanapotumia wanga sana.

 

MAGONJWA YANAYOWAKABILI

-          Rehemu mbaya (CHOLESTEROl)

-          Shohamu kwenye ini (BLOOD FAT NA LIVER FAT)

-          Shinikizo la damu na magonjwa ya moyo

-          Msongo wa mawazo

-          Saratani ya kizazi na utumbo

-          Magonjwa ya njia ya mkojo

-          Malaria maana ni maadui wa mbu

-          Kuishiwa damu (ANEMIA) n.k.

MAKUNDI YA DAMU - TABIA GROUP ‘B’

-          Ni kundi lenye tabia ngumu na ya kuasi sio rahisi kuwatawala (control)

-          Wana kazi na maono makubwa ila hawana ngumu ya kusimamia maono yao.

 

MAZURI KITABIA

-          Wana kasi ya utendaji

-          Ana uwezo wa kuishi na kundi lolote isipokuwa B mwenzake

-          Wanapenda raha na wana hisia nzito

-          Huiburudisha jamii na familia

-          Anaweza kumudu mazingira yeyote.

-          Hawatunzi kisasi muda mrefu.

 

MADHAIFU KITABIA

-          Wanakwepa majukumu sana kwa vitendo ila kwa maneno ni watendaji

-          Ni wasumbufu sana kwenye ahadi pia hawalipi madeni.

-          Wana hasira za haraka na ghafla

-          Wachonganishi

-          Ni ngumu kushirikiana nao.

-          Ni wasengenyaji kwa asili.

-          Ni wakali kwa watu wanaowaona wako chini yao.

 

KIJAMII

-          Hawapendi kushirikiana na wengine (wabinafsi)

-          Hawana msimamo hubadilikabadilika

-          Hawatakiwi kuwa viongozi ila watendaji

-          Anafaa sana kuwa watangazaji / mama maana hupenda kuonekana.

-          Jamii huwaamini sana wanaweza kujieleza

 

MAHUSIANO NA MAPENZI

-          Huwafurahisha wapenzi wao ila panahitajika uvumilivu maana wana hasira za haraka

-          Hukwepa majukumu ya kutunza na kutoa huduma kwa mwezi

-          Ni wakali, wakatili

-          Anachosema chaweza kisiwe kiicho moyoni (ni wadanganyifu)

-          Hawatulii na mtu mmoja katika kutoka kimahusiano (makahaba wengi hutoka kundi hili)

-          Sio wapenzi wazuri sana maana hupenda k+ualiti na hutumia usaliti ili kuwaumiza wapenzi wao

-          Kupenda kutoa na kupokea rushwa ya ngono nk.

 

KIAFYA

-          Wana kinga imara ya mwili hivyo hukabili magonjwa mengi, hata HIV hawatesi sana kama makundi mengine.

 

VYAKULA VINAVYOHITAJIKA KWAO

-          Maziwa, Siagi, Asali, Ngano, Soya, Samaki, Wali kwa ujumla ndilo kundi lililo na uwezo wa kutumia aina nyingi za vyakula.

 

VYAKULA VISIVYOHITAJIKA KWAO

-          Karanga, korosho, nyanya, pombe n.k.

 

MAGONJWA YANAYOWASHAMBULIA

-          Kuwa machizi, uvimbe wa fizi utumbo kufunga, saratani ya koo, kisukari aina ya pili Maralia uharibu ubongo, kibofu cha mkojo na kutoa harufu mdomoni.

 

ZIADA KWAO

-          Hawasumbuliwi na kipindupindu

-          Hawana msamaha wa kweli

-          Wanapokusaliti hupata Amani sana.

 

MAKUNDI YA DAMU KUNDI A-B

-          Hili ni kundi la mwisho na lililovumbuliwa hivi karibuni

-          Hili pia kundi lenye haiba mchanganyiko kama vile uoga, aibu, kuongozwa na wengine mitoko ya kuiga kwani hawako wazi kabisa.

 

MAZURI KITABIA

-          Ni rahisi kuwa marafiki

-          Wanachokuliana na mazingira kirahisi

-          Kila mmoja humtaka kuwa nae

-          Wanafikiri sana na wana akili nyingi

-          Ni wazuri sana kwa mambo hasa ya fedha maana akishika eno la fedha hufanya vizuri.

 

MADHAIFU YAO KITABIA

-          Ni wagumu kufanya maamuzi

-          Wanasahau sana

-          Wana hisia za kuyumba

-          Wapinzani, wabishi na wakosoaji

-          Wana dharau sana

-          Hufanya mambo taratibu

-          Hutoa wachoyo wengi.

KIJAMII

-          Hutumia akili kuishawishi jamii na anaminika sana kwa hoja zake

-          Ni mzuri kujieleza na kuonyesha udhaifu wa mambo ya wengine

-          Hutumia udhaifu wa wengine kunufaika

-          Ndilo kundi hutoa wanasiasa wazuri

-          Sio matajiri sana maana ni wachumi na huogopa hasara.

SIFA PEKEE

-          Ni wachache sana duniani

-          Hawatoi damu kwa kundi lolot isipokuwa wao

-          Wana kiburi na dharau (maana hujiamini sana)

KAZINI

-          Huwafurahisha wengine

-          Huwaangusha wengine kirahisi maani ni wabinafsi

-          Idara ya fedha ikiongozwa na kundi hili familia au taasisi haiwezi kupata hasara kirahisi.

 

MAHUSIANO

-          Huwafurahisha wenzi/wapenzi wao

-          Hupenda kukosoa pale anapoona makosa

-          Hupenda kupewa wao kwanza (wanapenda ofa ziwaelekee wao tu)

-          Kwenye kujamiana hupenda kuhudumiwa tu

-          Mabinti wa kundi hili huogopwa sana na wanaume maana wanajisimamia.

-          Akitoa ahadi kwenye mahudiano sio mzuri kuitimiza, maana wanasahau sana maana wana vitu vingi kichwani.

 

KIAFYA

-          Hushambuliwa sana na KIHAUSI, magonjwa karibia yote ya moyo, dengue, mafuta kujaa kwenye mishipa ya dmau na wazee wengi wa kudni hili hupoteza uwezo wa kufikiri (Tahira)

 

VYAKULA

-          Chakula muhimu kwao ni vile vinavyohitajika katika makundi ya A na B pia huepuka vyakula vya kundi O.

 

 

GROUP (O) NA TABIA ZAKE

Ni Kundi lenye sifa za kipekee pia kwa mfano huongezea makundi yote damu.

-          Hupenda maendeleo

-          Ni marafiki wazuri

-          Hutoa msamaha wa kweli

-          Ni wadadisi sana

-          Ni watoaji sana

-          Wana mtazamo chanya

-          Hutisha watu pale anapokuwa kiongozi.

 

MADHAIFU YAO KITABIA

-          Hupenda Fujo

-          Hupenda sifa

-          Kwao ni rahisi kukwepa majukumu

-          Ni ving’ang;anizi ili atimize atakacho

-          Wana kiburi liwalo na liwe

-          Wapenda fujo na ni wababe

-          Wana tabia za kijeshi

 

MAISHA KIJAMII

-          Ni marafiki wazuri

-          Ni wawazi sana

-          Ni wazenguaji maana hupenda kuudhi

-          Huanzisha mgomo na fujo, kuita maandamano

-          Hujitolea kuumia ili wengine wanufaike

-          Hutaka asikilizwe yeye tu

 

SIFA ZA PEKEE

-          Hupenda michezo sana

-          Anapokula nyama hujisikia furaha sana

-          Huzarisha aside nyingi sana

MAHUSIANI YA MAPENZI

-          Huonyesha mapenzi wazi na kutaka kuwa wazi

-          Hutaka apendwe kama anavyopenda

-          Wanaume wa kundi hili hupenda wanawake wenye makario makubwa

-          Hutoa hofu sana kwa wapenzi wao wapya

-          Ni wahongaji sana

-          Hunogewa na wapenzi wapya

-          Hutelekeza familia kwa ajili ya wapenzi wapya

 

KIAFYA

-          Wana kinga ya kutosha dhidi ya kipindupindu.

-          Hawana kinga dhidi ya TB na Malaria

 

     MAGONJWA YANAYO WASUMBUA

-          Saratani ya kongosho, utumbo, kizazi

VYAKULA VINAVYOTAKIWA KWAO

-          Vyakula vya protini, hasa wanaume, mbogamboga majani, maji mengi, papai, tikitimaji, ndizi, nanasi n.k.

                VYAKULA VISIVYOTAKIWA KULA

-          Wanga, maembe mabichi, maharage ya njano, ukwaju, machungwa, juisi mulalo, wali sana na mahindi meupe n.k. Wanawake wa kundi hili huathirika Zaidi na vyakula hivyo.

 

MAMBO YA MUHIMU KUJUA PIA.

Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa:-

-          Kundi AB ndilo kundi lenye uwezo mkubwa wa akili likifuatiwa na kundi A, kisha kundi O NA MWISHO KUNDI b.

-          Hii ilifanyiwa utafiti na chuo kikuu cha JERASH – JORDAN Mwaka 2014.

-          Kila kundi la damu lina athari hasi kwa jingine na athari chanya hivyo yote ni bora.

-          Mimea na viumbe vitumikavyo kwa chakula vina DNA, zinazoendana au kuelewana na DNA za binadamu, inapotokea kula vyakula vyenye DNA kinzani basi inabidi yatokee mabadiliko ya KITABIA, KIAFYA NA KIROHO.

-          Hivyo maandiko ya Mwenyezi Mungu yanapozuia kutumia viumbe Fulani huwa ina maana kubwa sana kimwili, kiroho na kiakili,

-          Pamoja na madhaifu ya sayansi bado sayansi imekuwa mkono wa Mwenyezi Mungu kutoa Elimu hivyo tunakubali japo tahadhari ni muhimu.

-          Kama ambavyo sayansi imesaidia kuboresha maisha na kutoa elimu bora ili binadamu aishi kwa furaha pia sayansi imetumika kuharibu kwa sehemu kubwa ya binadamu.

-          Msisitizo tunahitaji sana sayansi na tunamhitaji sana Mungu.

-          Mfano sayansi imetupa vifaa tiba, uvumbuzi wa magonjwa nk. Lakini sayansi hiyo hiyo inatengeneza kemikali za kuua watu, wanyama na viumbe hai.

-          Unaposoma jalida hili pia omba Mungu akuepushe na zile tabia zinazowaathiri wengine.

 

No comments:

Post a Comment