Saturday, February 10, 2024

TED WILSON AWATAKA VIONGOZI WA KANISA WASIO NA IMANI JUU YA BIBLIA KUJIUZULU - OKTOBA 7, 2023

TED WILSON AWATAKA VIONGOZI WA KANISA WASIO NA IMANI JUU YA BIBLIA KUJIUZULU - OKTOBA 7, 2023

Na Gerry Wagoner

 Ifuatayo ni nakala ya mahubiri ya Sabato October 7, 2023 ya Ted Wilson  katika Baraza kuu la GC

 Kuna mambo kumi na sita (16) yaliyotolewa, na namba tatu ilihusu ngono ya kibiblia na uvamizi wa LGBTQ+ katika Uadventista. Mwishoni mwa hotuba yake kuhusu LGBTQ+, alihutubia viongozi, wachungaji, walimu, wanatheolojia, watoa huduma za afya, na washiriki wa kanisa, wakiwemo wale wanaotazama mtandaoni.

  Ikiwa huwezi kwa sababu fulani kutokiamini kikamilifu kitabu hiki (Biblia), kama huwezi kulikubali Neno la Mungu jinsi linavyosomwa, ninakusihi ujiuzulu nafasi yako (makofi makubwa yalijaa chumbani). Tunataka viongozi wanaoamini Neno la Mungu 100%” (makofi zaidi)._*

  Haya hapa Mahubiri kamili ya Sabato - Ted Wilson, "Ukienda kwenye mtandao, unaweza kusikia kila aina ya mambo ya ajabu-kuhusu mimi. Hatuna wasiwasi kuhusu hilo. Kwa sababu tumechaguliwa kwa misheni. Tuna upinzani wa ndani na wa nje na kudharau Neno la Mungu. Mtasikia zaidi kuhusu hilo asubuhi ya leo—kudhalilishwa na kutokubalika kwa Neno la Mungu, na kila aina ya mashambulizi mengine ya hasira, ikiwa ni pamoja na madai ya uwongo dhidi ya kazi ya Mungu. Watu mbalimbali hupotosha ukweli na kupotosha tabia ya kanisa la Mungu. Baadhi ya watu wamebobea katika hilo. Wanaishi ili kuwafanya wengine waonekane wabaya. Washiriki wa kanisa letu ulimwenguni kote, wakiwakilishwa na divisions kumi na tatu za ulimwengu, wanachanganyikiwa kuhusu mienendo ya jamii na changamoto kwa Neno la Mungu. Na usumbufu huu wa kutatanisha unaharibu utume wa Mungu tuliokabidhiwa kwa kanisa la SDA. Kwa dakika chache, hebu tuangalie baadhi ya changamoto [katika kanisa letu] na baadhi ya majibu ambayo yatatuelekeza tena kwenye utume kamili wa kanisa. Vitu vingi tutakavyoviangalia vinahusika katika Ulimwengu wa Waadventista. Watu wanahitaji kujua. Pia tunatayarisha video fupi ili kuwasaidia washiriki wetu ulimwenguni pote kujua ukweli wa Biblia, na msimamo wetu kuhusu masuala. Na kwamba tunazingatia agizo la Mungu kwa kuwa tumechaguliwa kwa utume maalum.

 HOJA 16 ZENYE CHANGAMOTO

Ukosefu wa ufahamu wa Biblia* jinsi ya kuifasiri na uadui dhidi ya Neno la Mungu. Kanisa la SDA linaamini katika uhalisi na mamlaka ya Biblia Takatifu na inapaswa kutumika kwa watu wote kila mahali, kwa wakati wote. Kanisa linakubali tu mbinu ya kihistoria ya kibiblia au ya kihistoria ya kisarufi ya kufasiri Maandiko, ikiruhusu Biblia kujitafsiri yenyewe kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Nataka uiweke akilini mwako, tunashambuliwa na mbinu nyingine za kufasiri Biblia. Mbinu hizo hazilengi kuleta utukufu kwa Mungu, bali ni za kibinadamu. Hazikubaliki kwa Waadventista Wasabato. Ndani ya hizo, mtu mwenyewe anakuwa mwamuzi wa kile ambacho ni kweli na kile ambacho sio kweli. Ninawasihi tutumie mbinu ya wanahistoria pekee unapotafuta kuelewa unabii wa Biblia. Sio mbinu ya MATUKIO YALIOKWISHA PITA, na sio ya MATUKIO yajayo (Futurism). *_“Katika siku za mwisho, dunia itakuwa karibu kukosa imani ya kweli” (SG 94)._* Usishawishiwe na watu katika kanisa la [SDA] wanaolidharau Neno la Mungu.” Tunaikubali kama inavyosomwa!” 

 Kuchanganyikiwa kuhusu Uungu na Utatu.* 

Baada ya mahubiri haya, wasaidizi wangu watapokea jumbe “Kwa nini Wilson alisema hivyo?” Amekosea,” Tunaamini kwamba kuna Mungu [Uungu] mmoja na Yeye anajumuisha Nafsi tatu za milele wanafanya kazi pamoja kwa umoja Imani ya Msingi #2 ni wazi Mungu huyu wa utatu anataka kututumia ili kusaidia kutekeleza mpango huu wa wokovu.

 Kutokuelewa Kuhusu Ujinsia WA Binadamu.*

Mada nyeti. Tunapaswa kuonyesha heshima na kujali watu wote, lakini Biblia iko WAZI juu ya maagizo ya Mungu kuhusu ngono ya binadamu. Biblia iko wazi kwamba ndoa ni kati ya mwanamume mmoja TU na mwanamke [wa kibaolojia]. Kubadilika katika ujinsia wa mwanadamu HAUKUBALIWI na Mungu. Sio tu LGBTQ, lakini pia uzinzi, uasherati, usagaji, ushoga, na mambo mengine yaliyo mbadala wa ngono. Hizo ni dhambi. Kumbuka, sisi sote ni wenye dhambi chini ya msalaba. Tunaposhughulika na hali hizi, shughulika kwa upendo, kwa staha na heshima, lakini jua kile ambacho Biblia inasema hasa. Kwa bahati mbaya, baadhi ya watu leo—hata ndani ya kanisa—tunafanya kazi na pande mbili na tawala zao ili kukabiliana na changamoto za sasa katika eneo hili la [LGBTQ+]. Ngoja nikuambie. Hakuna hata mmoja wetu katika migawanyiko yote ya ulimwengu ambaye ana kinga dhidi ya hili. Watu wengine wanageuza Neno la Mungu, kama vile Warumi 1:18-32. Watu wengine wanatetea kwamba Warumi 1 inasema kile ambacho haisemi. Soma Biblia kama inavyosomeka. Kanisa la ulimwenguni pote la SDA halikubali na halitakubali watu binafsi kama washiriki wa kanisa au viongozi wa kanisa waliochaguliwa ambao hawazingatii maagizo ya Biblia kuhusu ngono kwa binadamu. Usikubali mtu yeyote anayetumia vibaya maagizo ya Biblia yanayopatikana katika Warumi 1, Mambo ya Walawi 18, 20 na maandiko mengine mengi. Unaona, Neno la Mungu linatuambia tusimame imara juu ya maagizo ya [Bwana] ametupa uhakika  kuhusu jambo hili na mambo mengine mengi. Kama ilivyo kwa mazoea yoyote ya dhambi yaliyoainishwa katika Maandiko, tunapaswa kuwasaidia watu wanaokuja kwenye makanisa yetu kupata msamaha kamili na maisha mapya chini ya msalaba (2 Wakorintho 5:17). Tunaweza kufanywa viumbe vipya katika Yesu [Amina]. 

 Kama vile Mark Finley anavyosema “Si tiba ya uongofu—katika maana ya kiufundi ya kukashifu inaelezwa kwamba tunaamini—ni ubadilishaji wa Biblia unaobadilisha maisha. Kama Willy Oliver anavyosema, ‘kanisa letu halipingani na mtu yeyote, tuko upande wa Neno la Mungu!’ Katika mikutano yetu ya awali, [GCDO] tulikumbushwa kwamba haki ya Kristo inayohalalisha na haki yake ya kutakasa haiwezi kutenganishwa kamwe. Tunamtumikia Mungu mwenye nguvu (Wakolosai 3:12). Ninasema maneno yafuatayo katika roho hiyo: Watu watajaribu kupindisha maneno ya Biblia. Wachungaji, walimu, wanatheolojia, wasimamizi, na hata washiriki wa kanisa wanajaribu kupindisha maneno ya Biblia. Paulo anatuambia tusiruhusu mtu yeyote atudanganye kwa njia ya falsafa na udanganyifu mtupu. Kaa karibu na Neno la Mungu. Tuna wanatheolojia wengi wa ajabu katika kanisa letu. BRI ni shirika la ajabu, nina imani nao kamili. Lakini kuna baadhi ya wanatheolojia ndani ya safu zetu wenyewe wanapotosha Neno la Mungu. Sio kama linavyosomeka. Kaa mbali nao! (Mithali 4.) *_Viongozi, wachungaji, walimu, wanatheolojia, watoa huduma za afya, na washiriki wa kanisa… na wale walio katika chumba hiki, na wale wanaotazama mtandaoni…ikiwa huwezi kwa sababu fulani kutoamini kitabu hiki (Biblia), ikiwa huwezi kuikubali. Neno la Mungu likisomwa nakusihi ujiuzulu nafasi yako. [MAKOFI]. Tunataka viongozi wanaoamini kwa 100% katika Neno la Mungu. [MAKOFI]._*

 Kuchanganyikiwa juu ya Huduma ya Patakatifu na Haki kwa Imani.*

Huduma ya patakatifu wa kidunia uliotolewa na Mungu kwa Musa ni nakala ya moja kwa moja ya kile kilicho mbinguni. Inaonyesha mpango kamili wa wokovu, kuonyesha upendo wa Mungu na dhabihu kuu ya Kristo. Huduma ya patakatifu pa duniani na mbinguni ni funguo za kuelewa mchakato wa wokovu unaojikita katika haki ya Yesu Kristo. SDA zinapaswa kuwa na makuu katika kumwinua Yesu na haki yake. Usiruhusu mtu yeyote kusema kwamba sisi ni washika sheria, tumejitoa kwa haki ya Kristo. Ni kiini hasa cha jumbe za malaika watatu. Mnamo 1844 Kristo aliingia katika chumba cha pili cha patakatifu pa mbinguni ili kuanza hukumu ya uchunguzi na sasa anafanya maombezi kama kuhani wetu mkuu. Yeye ndiye njia yetu pekee ya uzima wa milele. Hatuokolewi kwa kuwa WALA MBOGA. Nancy na mimi tujaribu kuwa wala mboga mboga na tumefaulu kwa kiwango cha 95%. Hakika sisi ni walaji mboga, ambayo ni nzuri na wewe ninakupa pia. Hatuokolewi kwa hilo. Hatuokolewi kwa zaka na sadaka zetu. Tunaokolewa kwa neema na uwezo wa Yesu Kristo pekee.

 Maoni Mabaya Kuhusu Uumbaji wa Kibiblia.*

Kanisa la SDA linaamini kwamba Mungu aliumba dunia hivi katika siku sita halisi (kama zilivyi siku zetu). Mimi binafsi naamini kulingana na Biblia na Roho ya Unabii kwamba dunia hii ina takriban miaka 6,000 tu. Sabato ya siku ya saba ni ukumbusho wa tukio hilo la ajabu.

 Mafundisho ya Uongo.*

Wapo wengi. Baadhi yao hupunguza utakaso. Harakati moja ya uwongo ambayo inazunguka vyuo vikuu vyetu na vyuo vikuu inaitwa Ukweli wa Upendo. Ina mafundisho ya uongo kuhusu utakaso na kuhesabiwa haki. Imetoka kwa-inapokelewa mara moja-kila wakati, ambapo SDA HATUAMINI HILO. Mungu anakupenda kwa hivyo usijali kuhusu tabia yako ... Upendo wa Mungu una nguvu sana lakini mafundisho haya ya uwongo ni hatari sana. Sikia hili. Kanisa la SDA linapitia kipindi cha kupepetwa hivi sasa. Usijaribiwe na mafundisho ya uwongo! 

 Kupoteza Hisia ya Uharaka katika Vuguvugu la Marejeo ya Kristo.*

Wengi wamepoteza hisia zao za uharaka na matumaini katika Ujio wa Pili wa Kristo. Kuzorota kwa sasa kwa ulimwengu unaotuzunguka kunapaswa kutuamsha tuone uharaka huo. Mara tatu katika Ufunuo 22, Yesu alionyesha kwamba anakuja upesi. Tuishi kwa hisia hiyo ya uharaka. Anguka chini ya msalaba na umruhusu Mungu akuandae kwa ujio wa pili wa Yesu Kristo. 

 Kupoteza Utambulisho kama Kanisa la waliosalia la Mungu.* 

Sisi ni waliosalia wa kanisa la Mungu, si tu dhehebu jingine. Tumeitwa kumwinua Kristo kwa kuhubiri jumbe hizo za malaika watatu—kuwageuza watu warudi kwenye ibada ya kweli ya Mungu. Sisi tuna harakati ya kipekee, yenye ujumbe wa kipekee kwa utume wa kipekee. Usichanganyikiwe kuhusu Ujumbe maalum wa Mungu. Ngoja nizungumze na Viongozi wote wa Union na konferensi zetu (139 kati yao), nyinyi ndio wenyeviti wa taasisi zetu za elimu. Jihadharini na yale yanayofundishwa katika taasisi hizo, hasa madarasa yetu ya dini. Tunahitaji kurekebisha na kuzitia nguvu upya taasisi zetu. 

 

Shutuma za Uongo kuhusu Uhusiano wa Kanisa na Ekumeni.*

Kanisa la SDA halihusiki katika harakati za uekumene (Umoja wa makanisa ya Jumapili)na mashirika au mienendo mingine ya kidini. Tunaamini katika kufanya urafiki na vikundi vingine vya kidini. Ninakutana na viongozi na viongozi wengi na kujaribu kuwa [karibu] kila mara kwa maombi na viongozi hawa wa umma tu.

 Changamoto kwa Mamlaka ya Kanisa.*

Kanisa limejengwa juu ya mfumo wa uwakilishi unaoongozwa na Roho Mtakatifu, na tunafanya maamuzi ya moja kwa moja katika chumba hiki. Maamuzi ya kanisa yanapofanywa katika ngazi ya dunia nzima juu ya maagizo ya Biblia na Roho ya unabii na kuongozwa na maombi, maoni binafsi yanapaswa kuwekwa kando. Wakati watu na taasisi zinaasi dhidi ya maamuzi ya pamoja ya kanisa, GC haiwezi tu kuwafukuza watu kazi au kufuta mashirika bila kupitia mchakato. GC sio eneo lenye mpangilio wa amri na udhibiti wa watu. Kuna hatua za kinidhamu hizo zinaweza kutumika lakini kanisa linafanya kazi ya kuwarudisha watu kwenye umoja. Biblia na Roho ya unabii zimejaa mwongozo kwamba tunapaswa kukubali maamuzi ambayo hufanywa na kanisa la ulimwengu katika vipindi maalum. [Tunapaswa kutumia zana tuliyounda kutatua matatizo haya.] 

 

Kutoelewa Kuhusu Roho ya Unabii.*

Kuna mashambulizi ya mara kwa mara kwenye Roho ya unabii, ambayo mwandishi EGW alitabiri katika maandishi yake. Yasome na yafuate maagizo yake.

 Ukosefu wa Kuelewa Maana ya Kweli ya Sabato ya Siku ya Saba.*

Inua utakatifu na kitakasa Sabato ya siku ya saba. 

 Mkanganyiko Kuhusu Hali ya Wafu.* Uchawi, mafumbo na umizimu vinakua sana. Sekta ya burudani inakuza umizimu.

 Mkanganyiko Kuhusu Ufahamu wa Kinabii wa Matukio ya Siku za Mwisho.* Baadhi ya watu hupuuza uelewa wa kinabii wa kihistoria wa kanisa la SDA. Mnyama kutoka baharini ni upapa na mnyama mwenye pembe mbili ni Marekani. Muungano wa utatu wa uprotestanti ulioasi, ni Ukatoliki wa Kirumi na umizimu unaokua na kutakuwepo na upotevu wa uhuru wa kidini kadri utunzaji wa Jumapili unavyotekelezwa. Mungu atawavusha watu wake katika wakati mgumu sana ulio mbele yetu.

 Ukosefu wa Shauku ya Uinjilisti na Ushuhudiaji.*

Shiriki imani yako kwa kila njia iwezekanavyo. Kataa mbinu ya Walaodikia ya kutofanya lolote.

 Kujitenga na Mtindo wa Maisha ya Kikristo na kuishi kama Ulimwengu.* Epuka mavazi ya kidunia, muziki, ulaji, burudani, na tabia n.k. Ni uchunguzi wangu kwamba Mungu anaanza kutikisa na kupepeta wana-vuguvugu la Marejeo. Hebu tuishi maisha safi na rahisi kulingana na Biblia. Vinginevyo sisi tunapita kama mawingu bila maji na miti isiyo na matunda (Yuda 12:13). Huu ndio ulimwengu ambao tunaishi sasa. Bila kujali usumbufu huu wenye kutatanisha, Mungu angali analilinda Kanisa la Waadventista Wasabato.” 

 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli; 14 aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. 15 Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu. 16 Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, 17 awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema. ”( 2 Wathesalonike 2:13-17 )_

 Imetafsiriwa na Pr Gibson MUJUNI Wilson ±255789982615

 

No comments:

Post a Comment